The Way 2 Life
  Je Mungu Anakupenda?
 
 

Swali: Wakati mwingine nakuwa na shaka kama kweli Mungu ananipenda. Kama yeye ni Mungu wa upendo, kwa nini basi kuna mateso na huzuni nyingi duniani?

Jibu: Katika kitabu cha Mungu kiitwacho BibliaMungu anaeleza bayana kuwa dhambi zetu ndio chanzo cha mateso na huzuni zote. Ni kweli kuwa Mungu anadhihirisha upendo wake kwa ulimwengu wote, kama tusomavyo katika sura maarufu sana ya biblia yaani Yohana 3: 16

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Pamoja na kuwa Mungu anadhihirisha upendo wake kwa ulimwengu, Mungu ana la ziada la kutuambia:

Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana. Bali humpenda mtu afuatiaye wema (Mithali 15:9)

Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, basi njia ya wasio haki itapotea        ( zaburi 1:6)

Swali: Lakini mimi sio mtu mwovu. Ni mwema na mwadilifu. Wema wangu unazidi ubaya wote niliowahi kufanya. Sasa, hii mistari inanihusu vipi mimi?

Jibu : Kwa viwango vya Mungu kuhusiana na haki, hata mtu mwadilifu kuliko wote, anatazamwa kama mwovu aelekeaye kuzimu. Biblia inasema ya kuwa hakuna mtu hata mmoja aliye mwema vya kutosha kwa matendo yake mwenyewe astahiliye kwenda mbinguni. Badala yake sisi sote tu waovu na tuna hatia ya dhambi mbele za Mungu.

Kama ilivyoandikwa ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.

Hakuna afahamuye, hakuna amtafutaye Mungu. ( warumi 3:10-11)

Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha;

nani awezaye kuujua? ( yeremia 17:9)

Swali: basi kama mimi ni mwovu kiasi hicho machoni pa Mungu, je Mungu atanifanya nini?

Jibu: Biblia inafundisha kuwa, siku ya mwisho, waovu wate watakuwa katika adhabu ya milele katika mahali panapoitwa Kuzimu.

Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu,unateketeza hata chini ya kuzimu,unakula dunia pamoja na mazao yake,unaunguza misingi ya milima. Nitaweka madhara juu yao chunguchungu; nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe; watakonda kwa njaa,wataliwa na makaa ya moto, na uharibifu mkali; nitawapelekea meno ya wanyama wakali, pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini. (Kumb. 32:22-24)

Swali : Ah! Acha utani bwana, kuzimu ni dhahania tu, si kitu halisi. Isitoshe mambo si mabaya kiasi hicho.

Jibu : Naam, Kuzimu ni halisi na mambo ni mabaya sana kwa kila mtu ambaye bado hajamkubali Yesu kama mwokozi wake. Biblia mara nyingi tu inazungumzia kuhusu kuzimu. Inafundisha kuwa kuzimu ni ya milele na ni mahali pa mateso makali.

Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto Ufunuo 20:15 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki. Na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio nakusaga meno

(Mathayo 13:49-50)

.....wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto, huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu, watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake. (II wathesalonike 1:7-9)

Swali : Hii ni hatari! Kwa nini sasa Mungu aliumba kuzimu?

Jibu : Kuzimu ni mahali pa kutisha. Kuzimu ipo kwa sababu Mungu alimuumba mtu ili awajibike mbele za Mungu kwa matendo yake.

Hukumu ya Mungu iliyo kamili inahitaji kila mtu kulipa kwa dhambi zake.

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti. Warumi 6:23

Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotendwa kwa mwili, kadri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. 2 wakorintho 5:10

Basi, nawaambia, kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Mathayo 12:36

Swali : Je, hiyo inaamaanisha kuwa katika siku ya mwisho kila mtu atafufuliwa ili ahukumiwe na kupelekwa kuzimu?

Jibu : Naam,inamanisha hivyo. Isipokuwa tu kama akiwepo mtu badala yetu atakayebeba mapigo yetu na adhabu yetu ya milele kwa sababu ya dhambi.Bahati nzuri yupo. Na huyo mtu ni Mungu mwenyewe aliyekuja duniani kama Yesu Kristo, ili abebe ghadhabu ya Mungu badala ya wote wanaomwamini.

Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja amegeukia njia yake mwenyewe; na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote. Isaya 53:6

Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.Isaya 53:5

Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko, na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu,kama yanenavyo maandiko. 1 wakorintho 15: 3-4

Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. 2 wakorintho 5: 21

Swali : Je, unasema kuwa kama nikimkubali Yesu kama aliyebeba dhambi zangu na kuwa aliadhibiwa kwa niaba yangu, sitakuwa na sababu ya kuendelea kuhofu kuhusu kuzimu?

Jibu : Ndio. Kama nimemwamini Yesu kuwa mwokozi wangu,ni sawa na kuwa nimeshasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Kristo kwa niaba yangu amekwisha kulipa deni ya dhambi zangu.

Amwaminiye Mwana yu na uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. Yohana 3: 36

Swali : Lakini ina maana gani kumwamini yeye? Ikiwa nakubaliana na yote biblia isemayo kuhusu Yesu kuwa mwokozi, sitakuwa na sababu ya kuwa na hofu ya kwenda kuzimu?

Jibu : Kumwamini Kristo kuna maana pana zaidi tu ya kukubaliana katika akili zangu na kweli za biblia. Inamaanisha kuwa ninakubaliana na ukweli wote wa maandiko, ambayo ni sheria ya Mungu kwangu. Na pia inamanisha kuwa nina hamu isiyokoma ya kutaka kuwa mtiifu kwa amri za biblia. Hivyo nakuwa na furaha kwa kutambua kuwa ninaishi kulingana na maelekezo ya Mungu kama yalivyo katika biblia.

Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.1 yohana 2: 3

Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, nakumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Mathayo 6: 24

Swali : Unamaanisha kwamba hakuna namna ya kuepuka kuzimu isipokuwa tu kwa kumwamini Yesu? Vipi kuhusu dini nyingine na hata baadhi ya zile zinazomkiri Kristo? Je, wafuasi wa dini hizo watakwenda kuzimu?

Jibu : Naam. Hawawezi kukwepa ukweli kuwa Mungu anatuwajibisha kwa sababu ya dhambi zetu. Dini nyingine haziwezi kutoa mkombozi kwa niaba ya wafuasi wake. Kristo ndiye pekee anayeweza kubeba hatia yetu na kutuokoa. Kwa hiyo imempasa kila mtu kuachana na dini yake na badala yake aiamini injili.

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matendo 4 : 12

Yesu akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Yohana 14: 6

Swali : Sasa nina hofu. Sitaki kwenda kuzimu. Nifanyeje?

Jibu : Hakuna lolote uwezalo kufanya ili kujiokoa. Biblia inatwambia ya kuwa ni Mungu pekee awezaye kukuokoa. Mungu anafanya muujiza wa wokovu kwa kutumia neno lake ( Biblia) ndani ya mioyo ya hao anaopanga kuwaokoa. Matokeo ya muujiza huu wa wokovu ndani ya muumini ni kuwa sasa ana upendo kwa Mungu na biblia. Anakuwa na furaha timilifu kwa kuitii sheria ya Mungu, biblia.Hivyo kama mtu kweli kabisa anahitaji kuokoka imempasa kutumia muda wa kutosha katika kusoma au kusikiliza biblia.

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Warumi 10 : 17

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu. Waefeso 2: 8

Mwanamke mmoja, jina lake Lidia ......akatusikiliza ( yaani paulo aliyemhubiria) ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana.... Mdo. 16:14

Swali : Unarudiarudia kuinukuu biblia. Ni ya muhimu kiasi hicho?

Jibu : Biblia ni kitabu cha muhimu kuliko vyote ulimwenguni,kwa sababu biblia ni sheria ya Mungu kwa wanadamu wote.Kwa kusoma au kuisikiliza biblia, mtu anajiweka katika nafasi nzuri ya kuokolewa na Mungu kama huo ni mpango wa Mungu kwa maisha yake. Kadhalika ataifunza ukweli wa kustaabisha kuhusu Mungu na mpango wake wa wokovu.Kimantiki anasikiliza sauti ya Mungu kwa kuwa Mungu ndiye mwandishi wa biblia na hivyo kwa kuisoma anazungumza naye kupitia neno lake(biblia).

Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha nafsi.Ushuhuda wa Bwana ni amini humtia mjinga hekima . zaburi 19:7

Heri walio kamili njia zao, waendao katika sheria za Bwana. Zaburi 119: 1

Swali : Je, ninaweza kumuomba Mungu anirehemu na kuniokoa?

Jibu : KABISA! Mungu ni mwenye rehema. Biblia inatuambia tunaweza na inatupasa kumuomba, kumlilia ili aturehemu na kutuokoa, huku tukitambua ya kuwa sisi ni waovu na tunastahili ghadhabu yake.

Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Luka 18: 13

Swali : Je, inanipasa kuhudhuria kanisani?

Jibu : Biblia inatuambia kwa karibu miaka 2000 baada ya Yesu kufa msalabani,hao waliomwamini Yesu,kama ingewezekana,iliwapasa kuwa washiriki wa kanisa.

Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu ( asomaye na afahamu ), ndipo walio katika uyahudi ( madhehebu ) na wakimbilie milimani ( Kwa Kristo )

Mathayo 24:15, 16.

Ni lazima tukumbuke kuwa hatuwezi kuokolewa na mchungaji, au kasisi, au ubatizo wa maje mengi, au kwa meza ya Bwana. Ni Yesu Kristo pekee ambaye ni Mungu, ndiye awezaye kutuokoa. Biblia inatufundisha kuwa wakati huu watu wengi wanokolewa nje ya kanisa.

Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao. Ufunuo 7: 9

Swali : Tafadhali nieleze zaidi jinsi Mungu aokoavyo watu.

Jibu : Biblia katika Yohana 11 inaonyesha ya kuwa ni Mungu pekee afanyaye kazi ya kuokoa. Kristo alimfufua mtu aitwaye Lazaro ambaye alikuwa kaburini kwa siku nne. Yesu alisimama nje ya kaburi la Lazaro na Kusema " Lazaro, njoo huku! " . Ni wazi kuwa maiti iliyooza ya Lazaro haingeweza kuisikia sauti ya Yesu wala kuitii. Biblia inatueleza ya kuwa kabla hatujaokoka tu wafu kiroho. Lakini Mungu anatuamuru tumtafute, tumwamini na tutubu. Hata hivyo, kama ilivyokuwa haiwezekani kwa Lazaro mfu kutii amri ya Yesu ya kutoka kwenye kaburi, haiwezekani kwa waliokufa kiroho kuiitii amri ya Mungu ya kumwamini Yesu kwa wokovu.

Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho yohana 6: 44

Lakini Lazaro aliisikia sauti ya Yesu na akatoka kaburini akiwa hai.Hii ilitokeaje?Inamaanisha ya kuwa Yesu alimwamuru Lazaro kutoka nje.

Yesu katika Roho wake aliingia katika kaburi na kuupa mwili wa Lazaro uliooza uhai wa kimwili, masikio ya kusikia, hiari pamoja na nguvu ya kutii amri ya Kristo.Vivyo hivyo kwa hao ambao Mungu amepanga kuwaokoa, anatuamuru tumwamini, tutubu, tuokolewe, anazungumza na maiti za kiroho ambazo kwa uwezo wao haziwezi kumtii Mungu. Kisha wako ambao wananza kumwamini Yesu kama mwokozi, ambao wanatambua kuwa wanapata furaha tu kama wakifanya mapenzi ya Mungu. Ushahidi upo katika maisha yao kwamba kwa namna fulani wameokoka. Hii imewezekana tu kwa sababu ,pale Mungu alipowaamuru kuokoka pia aliingia katika maisha yao na kuwawezesha kuokoka.Baada ya kuokoka wanajikuta kuwa wanachukia dhambi. Ni dhahiri kuwa Mungu aliwachagua ili waokoke. Kama bado haujaokoka, sikiliza biblia kwa makini sana.Kwa makini na kwa hali ya maombi soma biblia. Inawezekana na wewe pia ukapokea wokovu kupitia Roho wa Mungu.

BILA KUJALI UOVU WAKO NA UCHAFU WA MAISHA YAKO.KWA REHEMA ZA MUNGU, WEWE PIA UNAWEZA KUOKOLEWA.

Lakini kumbuka ya kuwa Mungu hufanya kila kitu kwa wakati wake. Kwa hiyo umsubiri Mungu kwa unyeyekevu wakati unaendelea kujifunza kutoka kwenye biblia.

Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana na kumngojea kwa utulivu maombolezo 3: 26

Kwa Mungu wokovu wangu, na utukufu wangu, mwamba wa nguvu zangu na kimbilio langu ni kwa Mungu.Enyi watu, mtumainini siku zote, ifufueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. Zaburi 62: 7,8

 
  Visitors 46 visitors (47 hits)